Sunday, 22 March 2015
TEZI DUME
TEZI DUME (PROSTATE GLAND)
Ni
tezi ambalo linapatikana kwa wanaume tu kwenye mifumo ya uzazi chini ya kibofu
cha mkojo.Kuna njia ambayo inaitwa urethra ambayo imeunganika kwenye uume
ambayo inapitisha mkojo kutoka nje.huwa inapitia kwenye tezi dume.Tezi dume ni
muhimu sana kwenye uzazi wa mwanaume kwa sababu huwa inazalisha fluid au
majimaji ambayo yanasaidia kulinda na kulisha mbegu za kiume .Mbegu hizi huwa
zinapitia mirija maalum ambayo inaitwa seminal vesicles kupitia ejaculatory
tract hadi kufikia urethra.
Tezi
dume huwa linachochewa kukaa katika hatua mbili tofauti:
(i)Tezi
dume huwa linachochewa na hormone (sex hormone)kutoka kwenye gololi za wanaume na kujenga
hisia……(ndio maana castration(kuasiwa)unakosa hamu ya tendo la ndoa.
(ii)Hatua
ya pili tezi dume huwa llinakua mwanaume anapofika umri wa miaka 30………
Wanaume
wengi huwa wanaanza mabadiliko au matatizo ya kwenda haja ndogo umri
unapoongezeka,ambayo huwa insababishwa na kutanuka kwa tezi dume,kumbuka
kutanuka kwa tezi sio tatizo ambalo linasababisha mtu kukosa kwenda haja ndogo
vizuri matatizo makubwa huwa ni cancer kwenye tezi.
DALILI
·
Kwenda
haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku.
·
Kukojoa
mara kwa mara wakati wa mchana.
·
Kutokwa
na mkojo bila kujizuiya.
·
Unaenda
kujisaidia haja ndogo lakini unachukua
muda mrefu mkojo kutoka.
·
Mkojo
unatoka tone kadhaa mara tu unapomaliza kwenda haja.
·
Unakojoa
karibu kiasi cha kuloanisha suruali.
·
Kusika
kibofu kizito au kinachoma wakati wa kukojoa
·
Kukojoa
kila baada ya muda mfupi.
MUONE
DAKTARI
·
Unapohisi
huwezi kukojoa.
·
Unaposikia
maumivu makali
·
Unapoona
damu kwenye mkojo.
·
Unapotokwa
na usaha au mbegu za kimu wakati wa kwenda haja ndogo
·
Kushindwa
kuzuia mkojo.
UVIMBE
WA TEZI DUME’
Bacteria
wakati mwingine huwa wanasababisha tezi dume kuvimba mtafute daktari.
·
Unaposikia
maumivu ya mgongo
·
Maumivu
chini ya kitovu
·
Kushindwa
kuzuiya mkojo.
Kinachosababisha
tezi dume kutanuka pia ni presha kupanda ,tezi dume linapotanukka au kukua
zaidi ya saizi ya kawaida,mwanaume huwa anapata shida kukojoa wakati mwingine
huwa wanatumia catheter.
Chanzo
kingine cha kuongezeka kwa tezi dume ni misuli ya urinary bladder kutanua au
kubadilika kuwa dhaifu.
EPUKA
NA :-
·
Kunywa
pombe,kahawa,vitu vya sukari n.k
UGONJWA WA HEMORRHOIDS/BAWASILI
UGONJWA WA HEMORRHOIDS/BAWASILI
Bawasili
ni ugonjwa ambao unatokana na nyama kuota sehemu za haja kubwa ndani au nje ya
haja kubwa.Ni mishipa ya damu (veins)ambayo huwa inavimba.Unaweza ukasikia
maumivu,muwasho au kutokwa na damu
nyeusi au mbichi au au usaha wakati mwingine kutoka sehemu hizo za haja
kubwa.tiba inategemea na dawa unazoweza kutumia,staili ya maisha yako au upasuaji.unapoona
tatizo linaongezeka muone daktari haraka.
CHANZO
NI NINI?
Bawasili
inasababishwa presha kubwa sehemu za haja kubwa (rectum)hii preha huwa
inatokana na:
·
Kufanya
mazoezi magumu kwa kukandamiza sana tumbo.
·
Kukosa
choo kwa muda mrefu(constipation)au kuharisha mara kwa mara kwa muda mrefu.
·
Upungufu
wa uzito au uzito kuongezeka(obesity)
·
Wakati
wa ujauzito(underweight).
·
Kuingiliwa
kinyume na maumbile(homosexual).
·
Kukosa
roughage
·
Kuumizwa
uti wa mgongo.
·
Staili
ya au kukaa ukiwa umeinama,.
Bawasili huwa inatokea kwa watu ambao mishipa ya damu
inatanuka sehemu za haja kubwa.
DALILI.
Dalili
huwa zinategemea na sehemu iliko bawasili.Inaweza iwe ndani ya haja kubwa au
nje ya haja kubwa.
Bawasili
ya ndani ya haja kubwa huwa inauma ndani kwa ndani na wakati mwingine
haitambuliki mapema.Lakini wakati wa kujisaidia haja kubwa inaweza ikachana ule
uvimbe na kutoa damu au muwasho sana.
Bawasili
ya nje huwa inajitokeza sehemu za haja kubwa kwa nje.huwa zinauma,kuwa au kutoa
damu.Bawasili za nje hutokana na damu kujaa kwa mishipa na kusababisha uvimbe
mkubwa,saizi ya yai la kuku.
BAWASILI
YA NJE UTAITAMBUA KWA:
·
Kupata
maumivu makali sehemu za haja kubwa wakati wa kukaa au kufanya mazoezi
·
Kupata
muwasho sehemu za haja kubwa.
·
Damu
mbichi zu nyeusi kwenye kinyesi
·
Uvimbe
sehemu za haja kubwa.
Dalili
za kutokwa na damu sehemu za haja kubwa ndo dalili mbaya sana kwa sababu
inaweza ikazalisha tatizo linguine kama saratani mtafute daktari.
·
Unapotokwa
na damu nyingi sehemu za haja kubwa.
·
Vidonda
vinapotokea sehemu za haja kubwa
·
Unatambua
kinyesi kuwa na damu nyeusi
TIBA
·
Muone
daktari
·
Tumia
cream lotion au osha sehemu hiyo na maji ya moto mara tatu kwa siku.
·
Tumia
dawa za maumivu kama paracetamol.
KUZUIA
·
Hakikisha
unapata choo kilaini.kukosa choo au kupata choo kigumu kunachangia sana tatizo
hili.
Mambo
yafuatayo yanaweza yakakusaidia kuepukana na bawasili.
·
Kula
vyakula ambavyo vina fibre(roughage)mboga za majani
·
Kunywa
maji ya kutosha
·
Unapoenda
haja kubwa usijikamue sana
·
Usikae muda mrefu ukiwa umezuia haja kubwa.
·
Pata
mazoezi ya kutosha
·
Epukana
na kukaa muda mrefu kila siku bila kunyanyuka.
MAGONJWA YA ZINAA
MAGONJWA YA ZINAA
MAGONJWA YA ZINAA
MAGONJWA YA ZINAA
MAGONJWA YA ZINAA
Magonjwa
ya zinaa ni magonjwa ambayo yanasambazwa kupitia kujamiiana.Mtu mmoja
aliyeambukizwa anaweza kusambaza kwa mtu mwingine ambaye hajaambukizwa.Yanawezwa
kuambukizwa kupitia ukeni au sehemu za haja kubwa kwa wale ambao wanajamiana
kupitia sehemuza haja kubwa.
VISABABISHI
VYA MAGONJWA YA ZINAA NI:-
·
Virus
kama HIV au hepatitis B
·
Bacteria
kama kisonono na kaswende,
Ni
nani ambaye anaweza kupata magonjwa haya?
Mtu
yeyote ambaye anajihusisha na kujamiiana na mtu mwingine ambaye ana magonjwa
haya.mf wa
·
Watu
ambao wana wapenzi wengi
·
Mtu
ambaye anamapenzi ambaye amewahi kuwa na wapenzi wengi.
·
Watu
ambao hawatumii condom wakati wa kujamiiana.
·
Watu
ambao wana wapenzi na hao wapenzi wana mahusiano sehemu nyingine na hawatumii
condom wakati wa kujamiiana.
·
Watu
ambao wanajiuza(wanaume na wanawake).
·
Watumiaji
wa madawa ya kulevya na hachukui tahadhari kwenye swala la kujamiiana.
DALILI
ZA STD
·
Dalili
huwa zanategemeana na aina ya maambukizi.mfano
·
Usaha
kutoka kwenye uume wa mwanaume au uke wa mwanamke.
·
Muwasho
mkali sehemu za siri.
·
Maumivu
makali wakati wa kujamiiana au waakati wa kwenda haja ndogo.maumivu yanawea
yawe ya kuchoma.
·
Upele
mwekundu unaweza kujitokeza sehemu za siri,haja kubwa,mdomoni,ulimi na kooni.
·
Maumivu
makali sehemu za haja kubwa wakati wa kujisaidia hususani wale ambao
wanajamiiana sehemu za haja kubwa.
·
Malengelenge
yanaweza yajitokeze sehemu za siri.
·
Wakati
mwingine ngozi ya mkononi na miguuni inaweza kutokkewa na mabakamabaka.
·
Mgonjwa
atapata homa kali,mwili kuchoka,nyama za mwili kuuma na matezi kujitokeza.
·
Maambukizi
kupitia hepatitis yanaweza yasababishi mkojo kuwa mzito au wa njano na kinyesi
kubadilika kwa rangi ya cheki nyeupe macho,kucha na ngozi hubadilika kuwa rangi
ya njano.
Kwa wale ambao wameambukizwa virusi vya ukimwi
wanaweza kupungua uzito wa mwili,maambukizi ya magonjwa ya mara kwa mara,jasho
usiku,kuchoka sana na upele au malengelenge kwenye ngozi na ulimi.n.k
Subscribe to:
Posts (Atom)