Sunday, 22 March 2015

MAGONJWA YA ZINAA

                                                         MAGONJWA YA ZINAA                

                                                               MAGONJWA YA ZINAA


MAGONJWA YA ZINAA
Magonjwa ya zinaa ni magonjwa ambayo yanasambazwa kupitia kujamiiana.Mtu mmoja aliyeambukizwa anaweza kusambaza kwa mtu mwingine ambaye hajaambukizwa.Yanawezwa kuambukizwa kupitia ukeni au sehemu za haja kubwa kwa wale ambao wanajamiana kupitia sehemuza haja kubwa.
VISABABISHI VYA MAGONJWA YA ZINAA NI:-
·        Virus kama HIV au hepatitis B
·        Bacteria kama kisonono na kaswende,
Ni nani ambaye anaweza kupata magonjwa haya?
Mtu yeyote ambaye anajihusisha na kujamiiana na mtu mwingine ambaye ana magonjwa haya.mf wa
·        Watu ambao wana wapenzi wengi
·        Mtu ambaye anamapenzi ambaye amewahi kuwa na wapenzi wengi.
·        Watu ambao hawatumii condom wakati wa kujamiiana.
·        Watu ambao wana wapenzi na hao wapenzi wana mahusiano sehemu nyingine na hawatumii condom wakati wa kujamiiana.
·        Watu ambao wanajiuza(wanaume na wanawake).
·        Watumiaji wa madawa ya kulevya na hachukui tahadhari kwenye swala la kujamiiana.
DALILI ZA STD
·        Dalili huwa zanategemeana na aina ya maambukizi.mfano
·        Usaha kutoka kwenye uume wa mwanaume au uke wa mwanamke.
·        Muwasho mkali sehemu za siri.
·        Maumivu makali wakati wa kujamiiana au waakati wa kwenda haja ndogo.maumivu yanawea yawe ya kuchoma.
·        Upele mwekundu unaweza kujitokeza sehemu za siri,haja kubwa,mdomoni,ulimi na kooni.
·        Maumivu makali sehemu za haja kubwa wakati wa kujisaidia hususani wale ambao wanajamiiana sehemu za haja kubwa.
·        Malengelenge yanaweza yajitokeze sehemu za siri.
·        Wakati mwingine ngozi ya mkononi na miguuni inaweza kutokkewa na mabakamabaka.
·        Mgonjwa atapata homa kali,mwili kuchoka,nyama za mwili kuuma na matezi kujitokeza.
·        Maambukizi kupitia hepatitis yanaweza yasababishi mkojo kuwa mzito au wa njano na kinyesi kubadilika kwa rangi ya cheki nyeupe macho,kucha na ngozi hubadilika kuwa rangi ya njano.
Kwa wale ambao wameambukizwa virusi vya ukimwi wanaweza kupungua uzito wa mwili,maambukizi ya magonjwa ya mara kwa mara,jasho usiku,kuchoka sana na upele au malengelenge kwenye ngozi na ulimi.n.k

1 comment:

  1. How to make the most of a casino? - Dr.MCD
    No, no. Casino Slots are casino games, and 남원 출장마사지 they aren't just for casual players. 광양 출장안마 Slot Machines are just 경기도 출장마사지 for beginners. Learn 창원 출장안마 How 문경 출장안마 to Play

    ReplyDelete