UGONJWA WA KICHOCHO/BILHARZIA
KICHOCHO/BILHARZIA
·
Ni
ugonjwa ambao unatokana na minyoo midogo ya aina ya schistosoma kuingia mwilini
na kusababisha muwasho katika viungo mbalimbali unaosababisha
homa,udhaifu,kupungukiwa ma kinga mwilini hadi kutokea kansa na kifo.
·
Minyoo
ya aina ya schistosoma inatokea katika konokono za maji kwa hali ya lava(larvae
stage)larvae zinatoka kwenye konokono na kutembea katika maji karibu nayo
zikitafuta wanyama au awtu wanapolenga kuingia ili waendelee kukua katika
miili yao.zinatoboa ngozi na kutembea na
kuingia hadi mishipa ya damu hadi maini
zinapobadilika kuwa minyoo yenye urefu wa milimita1-2,minyoo inaendelea
kutembea mwilini hadi kufikia utumbo,mapafu au ubongo.Huwa zinasababisha vurugu
katika viungo hivi na kusababisha mzio unaonekana kwa njia ya homa .Minyoo
inataga mayai yanayotoka mwilini kwa njia ya kibofu na mkojo.
·
Kama
mkojo unaachishwa kwenye maji,mayai hubadilika kuwa larvae zinazoingia katika
konokono na mzunguko unaanza upya.
·
Kwa
hiyo njia ya kuambukizwa ni kuingia
katika maji penye konokono zilizoambukizwa..siku hizi karibu kila ziwa,bwawa au
maji ya vidimbwi huwa na hatari ya kichocho.
DALILI
Kichocho
ni ugonjwa ambao ni chronic.wagonjwa wa kichocho huwa wanakabiliwa ana anemia
na utapia mlo.kichocho kinaweza kuonekana wiki chache baada ya maambukizi.
·
Utasikia
tumbo linauma sana
·
Kikohozi
kisichoisha
·
Kuharisha
mara kwa mara (damu)
·
Homa
kali
·
Kizunguzungu
·
Ini
kuvimba pamoja na bandama
·
Ongezeko
kubwa la seli nyeupe
·
Maambukizi
kwenye ngozi ambayo yanasababisha muwasho miguuni na sehemu zingine za mwili.
·
Muwasho
sehemu za siri na kutokea vidonda ambavyo vinaweza kuwa njia kuu ya maambukizi
ya ukimwi.
·
Mayai
yanaweza kusambaa hadi uti wa mgongo na kusababisha ugonjwa wa akili
·
Wakati
mwingine ugonjwa huu unasababisha uvimbe kwenye kizazi,matokeo yake mgonjwa
anapata
Presha ya kupanda au
kushuka,matatizo ya figo.
0 comments:
Post a Comment