FAIDA ZA MACHUNGWA
·
Ni
msimu mwingine wa machungwa ,yamejaa tele kila kona .sh 100 tu unapata chugwa
lakini sio ajabu kama kuna watu msimu unaisha hawajala hata chungwa moja wala
suala la matunda halipo kabisa katika
arodha ya milo yao.
·
Inawezekana
pia hata kwa wale wanaokula japo kidogo
hula kama kiburudisho tu bila kujua
faida zake mwilini, katika nakala ya leo nitakujuza faida 13 unazoweza kuzipata
unaokula chungwa ambalo limesheheni virutubisho kibao.
·
Kumbuka
kuwa hata chugwa moja tu ukila linakidhi yale mahitaji muhimi ya mwili ya kila
siku (daily requirements)iwe chugwa lenyewe au juisi yake halisi.
1. UKOSEFU WA CHOO
·
Kutokana
na kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre)chugwa
husaidia usagaji wa chakula tumboni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye ukosefu wa choo.Aidha
kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini,hivyo
chugwa ni zuri kwa wagonjwa wa sukari.
2. UGONJWA WA MOYO
·
Kiwango
kikubwa cha vitamin C na virutubisho vya (flavonoids)phytonutrients,vilivyomo
kwenye chugwa huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya
moyo(cardionascular diseases).
3. SHINIKIZO LA DAMU
·
Virutubisho
vya magnes (magnesium) na hesperidin vilivyomo kwenye chungwa husaidia kuondoa
tatizo la shinikizo la damu la juu(high blood presure) hivyo machugwa ni mazuri
kwa wagonjwa wa presha.
4. UGONJWA WA MAPAFU.
·
Chugwa
pia lina kiasi kikubwa cha vitamin B6 na madini ya chuma (iron)ni rutubisho
ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya
oksijen mwilini hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.
5. MIFUPA NA MENO
·
Chungwa
lina kiasi kingi cha madini ya halisi calcium ambayo ni muhimu kwa uimarishaji
wa mifupa na meno.
6. AFYA YA NGOZI
·
Art.oxdant
iliomo kwenye chugwa hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kutokana na
mabadiliko ya hali ya hewa pia huifanya ngozi isizeeke.
7. KOLESTRO
·
Virutubisho
vilivyomo kwenye chugwa hasa kwenye maganda yake hupunguza kiwango cha mafuta
mabaya mwilini (bad cholestol)hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa
kula machugwa pamoja na nyama zake.
8. UKUAJI WA UBONGO
·
Chugwa
moja lina kiasi cha silimia 10 ya folis acial inayohitajika mwilini kila siku madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi
na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa
kufikiri.
9. KINGA YA MWILI
·
Vitamin
C iliyomo kwenye chugwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu
kwa uimarishaji wa kinga ya mwili unapokuwa na kinga imara huwezi kushambuliwa
na magonjwa mara kwa mara yakiwemo malaria.
10.
UGONJWA
WA FIGO
·
Ulaji
wa machungwa mara kwa mara hutusaidia kujiepusha na ugonwa wa figo kwa kiasi
kikubwa .
11.
VIDONDA
VYA TUMBO
·
Unapokuwa
na kiwango cha kutosha cha vitamin C mwilini una uhakika wa kinga dhidi ya
ugonjwa wa vidonda vya tumbo na kama tayari unavyo ulaji wa machungwa utakupa
ahueni
12.
UGONJWA
WA MAFUA
·
Kutokana
na wingi wa virutubisho vilivyomo kwenye chugwa ulaji wake mara kwa mara
utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza na
vairas(virus/kama vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi hivyo kwa
machungwa mengi kadiri uwezavyo ili ujiepushe na mafua.
13.
KINGA
YA MAGONJWA MENGI
·
Chugwa
sio tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyo hapo
juu bali pia hutoa kinga kwa magonjwa mengine kama vile baridi
yabisi(arthritis rheumalism)pia kikohozi ,kifua kikuu nimonia na kisukari
nakushauri kula machugwa au juice yake halisi kuanzia leo hii kupata faida
hizo.
0 comments:
Post a Comment