UGONJWA WA HEMORRHOIDS/BAWASILI
Bawasili
ni ugonjwa ambao unatokana na nyama kuota sehemu za haja kubwa ndani au nje ya
haja kubwa.Ni mishipa ya damu (veins)ambayo huwa inavimba.Unaweza ukasikia
maumivu,muwasho au kutokwa na damu
nyeusi au mbichi au au usaha wakati mwingine kutoka sehemu hizo za haja
kubwa.tiba inategemea na dawa unazoweza kutumia,staili ya maisha yako au upasuaji.unapoona
tatizo linaongezeka muone daktari haraka.
CHANZO
NI NINI?
Bawasili
inasababishwa presha kubwa sehemu za haja kubwa (rectum)hii preha huwa
inatokana na:
·
Kufanya
mazoezi magumu kwa kukandamiza sana tumbo.
·
Kukosa
choo kwa muda mrefu(constipation)au kuharisha mara kwa mara kwa muda mrefu.
·
Upungufu
wa uzito au uzito kuongezeka(obesity)
·
Wakati
wa ujauzito(underweight).
·
Kuingiliwa
kinyume na maumbile(homosexual).
·
Kukosa
roughage
·
Kuumizwa
uti wa mgongo.
·
Staili
ya au kukaa ukiwa umeinama,.
Bawasili huwa inatokea kwa watu ambao mishipa ya damu
inatanuka sehemu za haja kubwa.
DALILI.
Dalili
huwa zinategemea na sehemu iliko bawasili.Inaweza iwe ndani ya haja kubwa au
nje ya haja kubwa.
Bawasili
ya ndani ya haja kubwa huwa inauma ndani kwa ndani na wakati mwingine
haitambuliki mapema.Lakini wakati wa kujisaidia haja kubwa inaweza ikachana ule
uvimbe na kutoa damu au muwasho sana.
Bawasili
ya nje huwa inajitokeza sehemu za haja kubwa kwa nje.huwa zinauma,kuwa au kutoa
damu.Bawasili za nje hutokana na damu kujaa kwa mishipa na kusababisha uvimbe
mkubwa,saizi ya yai la kuku.
BAWASILI
YA NJE UTAITAMBUA KWA:
·
Kupata
maumivu makali sehemu za haja kubwa wakati wa kukaa au kufanya mazoezi
·
Kupata
muwasho sehemu za haja kubwa.
·
Damu
mbichi zu nyeusi kwenye kinyesi
·
Uvimbe
sehemu za haja kubwa.
Dalili
za kutokwa na damu sehemu za haja kubwa ndo dalili mbaya sana kwa sababu
inaweza ikazalisha tatizo linguine kama saratani mtafute daktari.
·
Unapotokwa
na damu nyingi sehemu za haja kubwa.
·
Vidonda
vinapotokea sehemu za haja kubwa
·
Unatambua
kinyesi kuwa na damu nyeusi
TIBA
·
Muone
daktari
·
Tumia
cream lotion au osha sehemu hiyo na maji ya moto mara tatu kwa siku.
·
Tumia
dawa za maumivu kama paracetamol.
KUZUIA
·
Hakikisha
unapata choo kilaini.kukosa choo au kupata choo kigumu kunachangia sana tatizo
hili.
Mambo
yafuatayo yanaweza yakakusaidia kuepukana na bawasili.
·
Kula
vyakula ambavyo vina fibre(roughage)mboga za majani
·
Kunywa
maji ya kutosha
·
Unapoenda
haja kubwa usijikamue sana
·
Usikae muda mrefu ukiwa umezuia haja kubwa.
·
Pata
mazoezi ya kutosha
·
Epukana
na kukaa muda mrefu kila siku bila kunyanyuka.
0 comments:
Post a Comment