UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo katika mwili unaohusika na
umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na
mwili.
Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio
'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo
mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru
'Rectum'.
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo
mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika
kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii
hutambulika kama 'Peptic ulcers'.
Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita
vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita
'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'
VINAVYOSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO
Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu.
Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda
vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs
husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers'
Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana
kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati
mkila denda/kunyonyana midomo.
Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza
vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi
kwenye utumbo.
Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.
Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza
maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu
madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa
hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa
na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda.
Chembe za urithi 'Genetics'. Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya
tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu
kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.
Uvutaji sigara/tumbaku. Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta.
Matumizi ya pombe/vilevi. Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/pombe.
Msongo wa mawazo 'Mental stress'. Msongo wa mawazo hausababishi vidonda
moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.
Monday, 2 March 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment