Sunday 22 March 2015

BRUCELLA




BRUCELLA
Ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unasababishwa na bacteria ambayo inaitwa brucella. Bacteria inaweza kusambaa kutoka kwa  wanyama kwenda kwa binadamu .hawa bacteria wanasambaa kwa wanyama tofauti tofauti kama ng’ombe,mbwa.nguruwe.kondoo,mbuzi,ngamia  na mbwa mwitu .Brucella iliyoko kwa wanyama haiwezi kutibiwa lakini kwa wanadamu inatibika.
Brucella kwa wanadamu huwa inatokea mtu anapogusana na mnyama ambaye ana hawa bacteria.Mara chache sana mtu aliyeambukizwa bacteria anaweza kuambukiza mwingine.wanyama ambao wananyonyesha na wana bacteria (brucella)wanaweza kuambukiza watoto wao.Brucella pia inaweza ikasambaa kupitia kujamiiana.
Bacteria inaweza ikaingia mwili wa mtu kupitia:-
·         Kidonda au mkwaruzo unao ruhusu bacteria kupita
·         Ukivuta hewa chafu ambayo ina bacteria.
·         Unapo kula au kunywa kitu ambacho kina wadudu  wa brucella mfano maziwa ambayo hayajachemshwa au nyama ambayo haijapikwa vizuri ikaiva.
·         Kusafiri sehemu ambazo zina bacteria wengi wa brucella.
·         Kufanya kazi machinjioni au bucha za nyama
·         Kufanya kazi sehemu ambazo ng’ombe wengi wanafugwa.
DALILI
·         Homa kali(kusikia baridi wakati wa jua kali kama vile una malaria.)
·         Kuumwa sana na mgongo.
·         Nyama za mwili kuuma sana
·         Kukosa hamu ya kula na kupungua  uzito.
·         Kumwa sana na kichwa,
·         Kutokwa na jasho wakati wa usiku.
·         Mwili kuchoka bila sababu.
Dalili zinaweza zikajitokeza ndani ya siku 30 baada ya kugusana na bacteria.
Matatizo yatokanayo na ugonjwa wa brucella
·         Huwa inaharibu mifumo ya mishipa ya fahamu mpaka mgonjwa kusikia ganzi kabisa.
·         Huwa inaathiri utendaji kazi wa moyo na valve zake(zinaweza zikatanuka)
·         Brucella inaweza ikasababisha kuvimba kwa ini.
·         Inasababisha matatizo  kichwani na mgonjwa kuchanganyikiwa.
·         Maumivu makali ya viungo.
·         Kwa wa mama wajawazito,inaweza ikasababisha mimba kuharibika.
Inaweza ikasababisha kilema kwa mtoto mchanga anayezaliwa.

3 comments:

  1. Mnapatikana wapi nasumbuliwa na huo ugonjwa.

    ReplyDelete
  2. Nenda hospital kapime kwanza. Kipimo chake tu 30k. Nimetoka kupima nipo naendelea na dozi...

    ReplyDelete
  3. Mtu mwenye brucella anweza kumwambukiza mtu kama mke au watoto

    ReplyDelete