Sunday 22 March 2015

FAIDA ZA MACHUNGWA

FAIDA  ZA MACHUNGWA

 




·         Ni msimu mwingine wa machungwa ,yamejaa tele kila kona .sh 100 tu unapata chugwa lakini sio ajabu kama kuna watu msimu unaisha hawajala hata chungwa moja wala suala la matunda halipo kabisa katika  arodha ya milo yao.
·         Inawezekana pia hata kwa wale wanaokula  japo kidogo hula  kama kiburudisho tu bila kujua faida zake mwilini, katika nakala ya leo nitakujuza faida 13 unazoweza kuzipata unaokula chungwa ambalo limesheheni virutubisho kibao.
·         Kumbuka kuwa hata chugwa moja tu ukila linakidhi yale mahitaji muhimi ya mwili ya kila siku (daily requirements)iwe chugwa lenyewe au juisi yake halisi.

1.   UKOSEFU WA CHOO
·         Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre)chugwa husaidia usagaji wa chakula tumboni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye ukosefu wa choo.Aidha kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini,hivyo chugwa ni zuri kwa wagonjwa wa sukari.
2.   UGONJWA WA MOYO
·         Kiwango kikubwa cha vitamin C na virutubisho vya (flavonoids)phytonutrients,vilivyomo kwenye chugwa huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo(cardionascular diseases).
3.   SHINIKIZO LA DAMU
·         Virutubisho vya magnes (magnesium) na hesperidin vilivyomo kwenye chungwa husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu(high blood presure) hivyo machugwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.
4.   UGONJWA WA MAPAFU.
·         Chugwa pia lina kiasi kikubwa cha vitamin B6 na madini ya chuma (iron)ni rutubisho ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu  ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksijen mwilini hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.
5.   MIFUPA NA MENO
·         Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya halisi calcium ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.
6.   AFYA YA NGOZI
·         Art.oxdant iliomo kwenye chugwa hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa  na magonjwa ya ngozi yanayoweza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa pia huifanya ngozi isizeeke.
7.   KOLESTRO
·         Virutubisho vilivyomo kwenye chugwa hasa kwenye maganda yake hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholestol)hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machugwa pamoja na nyama zake.


8.   UKUAJI WA UBONGO
·         Chugwa moja lina kiasi cha silimia 10 ya folis acial inayohitajika mwilini kila  siku madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa kufikiri.

9.   KINGA YA MWILI
·         Vitamin C iliyomo kwenye chugwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili unapokuwa na kinga imara huwezi kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara yakiwemo malaria.
10.   UGONJWA WA FIGO
·         Ulaji wa machungwa mara kwa mara hutusaidia kujiepusha na ugonwa wa figo kwa kiasi kikubwa .
11.   VIDONDA VYA TUMBO
·         Unapokuwa na kiwango cha kutosha cha vitamin C mwilini una uhakika wa kinga dhidi ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo na kama tayari unavyo ulaji wa machungwa utakupa ahueni
12.   UGONJWA WA MAFUA
·         Kutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo kwenye chugwa ulaji wake mara kwa mara utakuepusha  na magonjwa ya kuambukiza na vairas(virus/kama vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi hivyo kwa machungwa mengi kadiri uwezavyo ili ujiepushe na mafua.
13.   KINGA YA MAGONJWA MENGI
·         Chugwa sio tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyo hapo  juu bali pia hutoa kinga kwa magonjwa mengine kama vile baridi yabisi(arthritis rheumalism)pia kikohozi ,kifua kikuu nimonia na kisukari nakushauri kula machugwa au juice yake halisi kuanzia leo hii kupata faida hizo.

0 comments:

Post a Comment