Sunday 22 March 2015

TEZI DUME


TEZI DUME (PROSTATE GLAND)
Ni tezi ambalo linapatikana kwa wanaume tu kwenye mifumo ya uzazi chini ya kibofu cha mkojo.Kuna njia ambayo inaitwa urethra ambayo imeunganika kwenye uume ambayo inapitisha mkojo kutoka nje.huwa inapitia kwenye tezi dume.Tezi dume ni muhimu sana kwenye uzazi wa mwanaume kwa sababu huwa inazalisha fluid au majimaji ambayo yanasaidia kulinda na kulisha mbegu za kiume .Mbegu hizi huwa zinapitia mirija maalum ambayo inaitwa seminal vesicles kupitia ejaculatory tract hadi kufikia urethra.
Tezi dume huwa linachochewa kukaa katika hatua mbili tofauti:
(i)Tezi dume huwa linachochewa na hormone (sex hormone)kutoka  kwenye gololi za wanaume na kujenga hisia……(ndio maana castration(kuasiwa)unakosa hamu ya tendo la ndoa.
(ii)Hatua ya pili tezi dume huwa llinakua mwanaume anapofika umri wa miaka 30………
Wanaume wengi huwa wanaanza mabadiliko au matatizo ya kwenda haja ndogo umri unapoongezeka,ambayo huwa insababishwa na kutanuka kwa tezi dume,kumbuka kutanuka kwa tezi sio tatizo ambalo linasababisha mtu kukosa kwenda haja ndogo vizuri matatizo makubwa huwa ni cancer kwenye tezi.


DALILI
·        Kwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku.
·        Kukojoa mara kwa mara wakati wa mchana.
·        Kutokwa na mkojo bila kujizuiya.
·        Unaenda kujisaidia haja ndogo lakini  unachukua muda mrefu mkojo kutoka.
·        Mkojo unatoka tone kadhaa mara tu unapomaliza kwenda haja.
·        Unakojoa karibu kiasi cha kuloanisha suruali.
·        Kusika kibofu kizito au kinachoma wakati wa kukojoa
·        Kukojoa kila baada ya muda mfupi.
MUONE DAKTARI
·        Unapohisi huwezi kukojoa.
·        Unaposikia maumivu makali
·        Unapoona damu kwenye mkojo.
·        Unapotokwa na usaha au mbegu za kimu wakati wa kwenda haja ndogo
·        Kushindwa kuzuia mkojo.
UVIMBE WA TEZI DUME’
Bacteria wakati mwingine huwa wanasababisha tezi dume kuvimba mtafute daktari.
·        Unaposikia maumivu ya mgongo
·        Maumivu chini ya kitovu
·        Kushindwa kuzuiya mkojo.
Kinachosababisha tezi dume kutanuka pia ni presha kupanda ,tezi dume linapotanukka au kukua zaidi ya saizi ya kawaida,mwanaume huwa anapata shida kukojoa wakati mwingine huwa wanatumia catheter.
Chanzo kingine cha kuongezeka kwa tezi dume ni misuli ya urinary bladder kutanua au kubadilika kuwa dhaifu.
EPUKA NA :-
·        Kunywa pombe,kahawa,vitu vya sukari n.k

0 comments:

Post a Comment