Sunday 22 March 2015

UGONJWA WA HEMORRHOIDS/BAWASILI

                                          




UGONJWA WA HEMORRHOIDS/BAWASILI
Bawasili ni ugonjwa ambao unatokana na nyama kuota sehemu za haja kubwa ndani au nje ya haja kubwa.Ni mishipa ya damu (veins)ambayo huwa inavimba.Unaweza ukasikia maumivu,muwasho au kutokwa  na damu nyeusi au mbichi au au usaha wakati mwingine kutoka sehemu hizo za haja kubwa.tiba inategemea na dawa unazoweza kutumia,staili ya maisha yako au upasuaji.unapoona tatizo linaongezeka muone daktari haraka.
CHANZO NI NINI?
Bawasili inasababishwa presha kubwa sehemu za haja kubwa (rectum)hii preha huwa inatokana na:
·        Kufanya mazoezi magumu kwa kukandamiza sana tumbo.
·        Kukosa choo kwa muda mrefu(constipation)au kuharisha mara kwa mara kwa muda mrefu.
·        Upungufu wa uzito au uzito kuongezeka(obesity)
·        Wakati wa ujauzito(underweight).
·        Kuingiliwa kinyume na maumbile(homosexual).
·        Kukosa roughage
·        Kuumizwa uti wa mgongo.
·        Staili ya au kukaa ukiwa umeinama,.
Bawasili  huwa inatokea kwa watu ambao mishipa ya damu inatanuka sehemu za haja kubwa.

DALILI.
Dalili huwa zinategemea na sehemu iliko bawasili.Inaweza iwe ndani ya haja kubwa au nje ya  haja kubwa.
Bawasili ya ndani ya haja kubwa huwa inauma ndani kwa ndani na wakati mwingine haitambuliki mapema.Lakini wakati wa kujisaidia haja kubwa inaweza ikachana ule uvimbe na kutoa damu au muwasho sana.
Bawasili ya nje huwa inajitokeza sehemu za haja kubwa kwa nje.huwa zinauma,kuwa au kutoa damu.Bawasili za nje hutokana na damu kujaa kwa mishipa na kusababisha uvimbe mkubwa,saizi ya yai la kuku.

BAWASILI YA NJE UTAITAMBUA KWA:
·        Kupata maumivu makali sehemu za haja kubwa wakati wa kukaa au kufanya mazoezi
·        Kupata muwasho sehemu za haja kubwa.
·        Damu mbichi zu nyeusi kwenye kinyesi
·        Uvimbe sehemu za haja kubwa.
Dalili za kutokwa na damu sehemu za haja kubwa ndo dalili mbaya sana kwa sababu inaweza ikazalisha tatizo linguine kama saratani mtafute daktari.
·        Unapotokwa na damu nyingi sehemu za haja kubwa.
·        Vidonda vinapotokea sehemu za haja kubwa
·        Unatambua kinyesi kuwa na damu nyeusi
TIBA
·        Muone daktari
·        Tumia cream lotion au osha sehemu hiyo na maji ya moto mara tatu kwa siku.
·        Tumia dawa za maumivu kama paracetamol.
KUZUIA
·        Hakikisha unapata choo kilaini.kukosa choo au kupata choo kigumu kunachangia sana tatizo hili.
Mambo yafuatayo yanaweza yakakusaidia kuepukana na bawasili.
·        Kula vyakula ambavyo vina fibre(roughage)mboga za majani
·        Kunywa maji ya kutosha
·        Unapoenda haja kubwa usijikamue sana
·        Usikae  muda mrefu ukiwa umezuia haja kubwa.
·        Pata mazoezi ya kutosha
·        Epukana na kukaa muda mrefu kila siku bila kunyanyuka.
 

0 comments:

Post a Comment