Monday 2 March 2015

VIDONDA VYA TUMBO

                                             UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO







Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo katika mwili unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili.
Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'.

Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'.
Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'
VINAVYOSABABISHA VIDONDA VYA TUMBO
Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu.
Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers'
Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo.
Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.
Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.
Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda.
Chembe za urithi 'Genetics'. Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.
Uvutaji sigara/tumbaku. Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta.
Matumizi ya pombe/vilevi. Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/pombe.
Msongo wa mawazo 'Mental stress'. Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.

0 comments:

Post a Comment