Sunday 22 March 2015

UGONJWA WA FIGO

                                              
                                                            UGONJWA WA FIGO
             


     FIGO
Ni kiiungo ambacho kinasaidia kuchuja uchafu kutoka kwenye damu.Ina kichujio ambacho kinaitwa glomerulus kinachuja uchafu na kupeleka kwenye kibofu cha mkojo kupitia mirija ambayo inaitwa ureters.
Zinasaidia pia kusawazisha shinikizo la damu kubalance mwili,kusawazisha chembechembe nyekundu katika mwili.

DALILI ZA UGONJWA WA FIGO
·      Ni malimbikizo ya uchafu(urea)kutoka mwilini na kujaa kwenye figo-huwa inasababisha:
1.  Udhaifu wa mwili,kukosa pumzi ,kuchanganyikiwa,figo kushindwa kuchuja urea(potassium) huwa inasababisha mapigo ya moyo kwenda mbio.
2.  Damu kwenye mkojo
3.  Kuumwa sana na tumbo chini ya  kitovu
4.  Mafua yasiyoisha
5.  Uzito wa mwili kuongezeka bila mpangilio
6.  Kuhema sana ukitembea hatua chache
7.  Kutokwa na jasho mara kwa mara.
8.  Kuwashwa mwili  mara kwa mara na kusikia kizunguzungu
9.  Miguu kuvimba,ukibonyeza ni kama papai lililoiva.
10. Pressure ya kushuka
11. Kukojoa mkojo wa njano,kukosa mkojo kabisa au kukojoa mdogo kwa kipindi .
12. Mawe kwenye figo(kidney stones)
13. Uric acid.
TIBA
· Kufanyiwa upasuaji au kubadilishiwa figo
· Kutumia dawa za kutibu figo
· Control ya blood pressure + kisukari maana vinachangia sana
· Epukana na ulaji mwingi wa chumvi au sukari.

0 comments:

Post a Comment